Baraza la Mawaziri laidhinisha marekebisho katika sekta ya Kidini

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais William Ruto aongoza mkutano wa Baraza la Mawaziri.

Baraza la Mawaziri limeidhinisha mkakati mpya unaonuia kubadilisha operesheni za mashirika ya kidini hapa nchini, mwaka mmoja baada ya kisa cha Shakahola kuibua mianya ya udhibiti katika sekta hiyo.

Hatua hii inafuatia mapendekezo ya jopo lililobuniwa na Rais kuhusu mashirika ya kidini, ili kuhakikisha maadili yanazingatiwa katika operesheni za kidini.

Katika mkutano ulioongozwa na Rais William Ruto siku ya Jumanne, Baraza hilo la Mawaziri liliidhinisha mapendekeza kadhaa kuhusu uhuru wa kuabudu na uwajibikaji kwa mashirika hayo ya kidini.

Baadhi ya mapendekezo hayo ni pamoja na kubuniwa kwa mikakati ya kudhibiti mashirika ya kidini, kubuniwa kwa Tume ya Maswala ya Kidini na kuimarishwa kwa mwavuli unaosimamia mashirika ya kidini ili kufanikisha ushirikishi.

Marekebisho hayo yatatekelezwa kupitia kundi la asasi mbali mbali litakalojumuisha vitengo vya usalama, jukwaa la dini mbali mbali na taasisi za elimu.

Jopo kazi hilo lilibuniwa na Rais kufanyia marekebisho mikakati  ya udhibiti wa mashirika ya kidini, kufuatia mauaji yaliyoshuhudiwa Shakahola.

Website |  + posts
Share This Article