Baraza la Chuo Kikuu cha Nairobi lamtimua Prof. Kiama

Dismas Otuke
1 Min Read

Baraza la Chuo Kikuu cha Nairobi limemtimua Profesa Stephen Kiama bila kutoa sababu zozote maalum.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa Baraza Kuu la Chuo Kikuu cha Nairobi Prof. Amukowa Anangwe kupitia kwa arifa ya Oktoba 14 huduma za Profesa Kiama zimesitishwa chuoni humo.

Kiama aliteuliwa Naibu Chansela wa chuo hicho Januari 5 mwaka 2020 kwa mkataba wa miaka mitano.

Tangu aliposhika hatamu za kukiongoza Chuo Kikuu cha Nairobi, Prof. Kiama amekuwa akilumbana na baraza la chuo hicho katika hatua ambayo imesababisha kutimuliwa kwake mara kadhaa.

Haijabainika ikiwa Prof. Kiama ataelekea mahakamani kupinga kutimuliwa kwake kama alivyofanya siku zilizopita.

Share This Article