Dkt. Barasa: Magonjwa ya Moyo kujumuishwa kwenye bima ya SHA

Tom Mathinji
1 Min Read
Hospitali ya matibabu ya magonjwa ya moyo ya Tenwek kaunti ya Bomet.

Waziri wa afya Dkt. Debora Barasa, ametangaza kuwa serikali imetoa kipaumbele kwa magonjwa ya moyo kujumuishwa katika bima ya afya ya jamii SHA, kama hatua ya kuimarisha mpango wa upatikanaji wa huduma za afya kwa wote UHC.

Akizungumza leo katika hospitali ya AGC Tenwek, kaunti ya Bomet wakati wa uzinduzi wa kituo cha kushughulikia magonjwa ya moyo, iliyoongozwa na Rais William Ruto, Dkt. Barasa alidokeza kuwa magonjwa ya moyo ni miongoni mwa chanzo kikuu cha maafa hapa nchini.

“Kuambatana na kujitolea kwetu kufanikisha mpango wa upatikanaji wa huduma za afya kwa wote UHC, tumetoa kipaumbele kwa magonjwa ya moyo kujumuishwa kwa bima ya afya ya jamii SHA, kuwafaidi waathiriwa wa ugonjwa huo,” alisema Barasa.

Waziri huyo alisema serikali imeboresha mfumo wa afya ya jamii kwa kutoa mafunzo kwa wahudumu wa afya ya jamii na kutekelezwa kwa mipango ya uchunguzi wa kiafya.

Hospitali hiyo ya AGC Tenwek, ndiyo ya kwanza iliyo nje ya Nairobi kutekeleza operesheni za moyo, huku operesheni 2,000 tangu mwaka 2008.

Share This Article