Barabara ya mzunguko wa Globe yafunguliwa

Dismas Otuke
1 Min Read

Mamlaka ya Kitaifa ya Barabara kuu nchini(KeNHA) imefungua barabara ya mzunguko wa Globe kuingia jijini Nairobi kwa matumizi ya wasafiri.

Barabara hiyo ilikuwa imefungwa tarehe 12 mwezi huu kupisha shughuli iliyokuwa ikiendelea ya kusafisha na ukarabati katika mto Nairobi.

Kwenye taarifa yake siku ya Jumatano, KeNHA ilisema barabara hiyo tayari imefunguliwa kwa matumizi ya wenye magari na wasafiri wengine.

Ufungaji wake ulisababisha msongamano mkubwa wa magari na hivyo kutatiza mno shughuli za usafiri katika eneo hilo.

Share This Article