Balozi wa Uingereza Neil Wigan atangaza kuondoka Kenya

Tom Mathinji
2 Min Read
Balozi wa Uingereza anayeondoka Neil Wigan.

Balozi wa Uingereza hapa nchini Neil Wigan, leo Jumatatu ametangaza kuodoka kwake hapa nchini mwishoni mwa mwezi Agosti, baada ya kuhudumu kwa muda wa miaka miwili.

Anaondoka hapa nchini kuchukua wadhifa mpya wa Mkurugenzi Mkuu wa mikakati katika afisi ya Mambo ya Nje ya Jumuiya ya Madola na Maendeleo Jijini London.

Huku akiangazia muda ambao amekuwa hapa nchini, balozi huyo alielezea huzuni kubwa kuondaka Kenya, huku aisifu ushirikiano ambao umeimarika kati ya Kenya na Uingereza katika biashara, uwekezaji, teknolojia, uvumbuzi na ubadilishanaji wa utamaduni, alizosema zimenufasha nchi hizo mbili.

“Tangu nilipowasili hapa nchini mwaka 2023, ushirikiano wa karibu wa mataifa haya mawili yalisababisha Mfalme Charles wa pili kuzu taifa hili, utiaji saini wa ushirikiano wa kimkakati kati ya Kenya na Uingereza, wanajeshi wa majini kupokea mafunzo kutoka Uingereza, uwekezaji katika miundombinu na mengine mengi,” alidokeza Wigan.

“Kenya na Uingereza zinaenda mbali, na imekuwa fahari yangu kuwa sehemu ya mafanikio hayo.  Asanteni sana na kwaherini.” alisema Wigan.

Kulingana na Wigan, atakayechukua nafasi yake atatangwa katika muda wa miezi kadhaa ijayo. Naibu balozi wa Uingereza nchini Kenya Dkt. Ed Barnett, atakaimu wadhifa huo.

Kabla ya kuja Kenya, Wigan alikuwa balozi wa Uingereza Nchini Israel kuanzia mwezi Juni 2019 hadi Juni 2023.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article