Bajeti 2024/25: Idara ya Mahakama yatengewa shilingi bilioni 24.7

Tom Mathinji
1 Min Read
I

Idara ya Mahakama imetengewa shillingi billioni 24.7 katika bajeti ya mwaka 2024-2025, iliyosomwa leo Alhamisi na waziri wa fedha na mipango ya kiuchumi Prof. Njuguna Ndung’u.

Akiwasilisha bajeti ya mwaka huu katika  majengo ya bunge, waziri wa fedha Prof. Njuguna Ndung’u, alisema shilingi milioni 900 zimetengwa kwa ujenzi na ukarabati majengo ya mahakama huku shillingi millioni 800 zikitengwa utekelezaji wa mpango wa idara hiyo wa kutoa huduma zake kupitia mtandaoni.

Katika bajeti hiyo, waziri huyo ametengea afisi ya Mkurugenzi wa mashtaka ya umma shillingi billioni 4, shillingi billioni 4.2 zikitengwa kwa tume ya maadili na kupambana na ufisadi EACC, shillingi billioni 6.9 kwa ofisi ya mwanasheria mkuu na shillingi billioni 8.7 kwa mkaguzi wa mahesabu.

Aidha waziri Ndung’u pia ametenga shillingi billioni 44.6 kwa bunge, akisema mgao huo unalenga kuimarisha utendakazi wa bunge.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *