Bafana Bafana ya Afrika Kusini ilinyakua nishani ya shaba katika makala ya 34 ya kipute cha AFCON, walipoilemea Leopards ya DR Congo penati 6-5 Jumamosi usiku.
Mechi hiyo iliamuliwa kupitia matuta ya penati moja kwa moja baada ya timu zote kuambulia sare tasa ndani ya dakika 90.
Chuo wa Congo watajilaumu baada ya kupoteza nafasi chungu tele na za wazi kufunga magoli, na kutawazwa washindi ndani ya dakika 90, huku wakidhihirisha mchezo mzuri na wa kusisimua.
Kipa wa Afrika Kusini Ronwen Williams alikuwa ngangari akipangua matobwe kadhaa ya moja kwa moja kutoka kwa Wakongo.
Ronwen alipangua penati mbili za Congo kati ya 7 zikiwa za Chancel Mbemba na Meshack Elia.
Ilikuwa mara ya pili kwa Afrika Kusini kumaliza ya taru latika kipute cha AFCON na ya kwanza tangu mwaka 2000.