Azimio watangaza maandamano Jumatano ijayo

Dismas Otuke
1 Min Read

Muungano wa Azimio One Kenya Alliance, umetangaza kuandaa maandamano Jumatano ijayo kote nchini kwa kipindi cha siku moja kuanzia saa kumi na mbili asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni.

Akitangaza maandamano hayo kupitia kwa kikao na wanahabari siku ya Jumamosi, kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka, amewarai wafuasi wao kufanya maandamano ya amani kuwa watulivu hata wakichochewa na polisi.

“Tunawaomba muwe watulivu hata mkichozwa na polisi mtulie ulimwengu mzima unatazama ,tunataka maandamano ya amani na msibebe silaha wala kuwajeruhi polisi.”akasema Kalonzo

Maandamano hayo ya kushinikiza serikali kupunguza gharama ya maisha na kusitisha utekelezaji wa matozo mapya yaliyopitiswa na serikali maajuzi.

Kumeshuhudiwa na visa vya uhuni,uharibifu wa mali ,makabiliano makali kati ya waandamanaji na polisi,majeruhi na maafa katika maandanamo ya siku tatu yaliyofanyika wiki hii.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *