Awamu ya pili ya zoezi la kuwahesabu wanyamapori yazinduliwa

Tom Mathinji
1 Min Read
Awamu ya pili ya zoezi la kuwahesabu wanyamapori kutekelezwa kaskazini mwa nchi.

Serikali ya taifa imezindua awamu ya pili ya zoezi la kuwahesabu wanyamapori, huku ikilenga eneo la kilomita 65,000 mraba katika kaunti sita za Kaskazini mwa Kenya.

Mradi huo unaongozwa na taasisi ya mafunzo na utafiti wa wanyamapori (WRTI), kwa ushirikiano na mashirika mengine 10.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo katika eneo la  Shaba, kaunti ya Isiolo waziri wa Utalii na Wanyapori Rebecca Miano, alielezea umuhimu wa zoezi hilo, akidokeza kuwa tangu zoezi lililofanywa mwaka 2021, taifa hili limekumbwa na ukame na mafuriko ambazo zimeathiri pakubwa wanyamapori.

Kulingana na waziri huyo, kuwahesabu wanyamapori ni muhimu kwa serikali kubuni sera za serikali na mikakati ya kukabiliana na majanga.

Taasisi ya WRTI, katika awamu ya kwanza ya zoezi hilo mapema mwaka huu, kwenye maeneo ya Mara, Amboseli, na Magadi, ilidokeza ongezeko la idadi ya ndovu kwa asilimia 29, huku idadi ya Nyati ikipungua.

TAGGED:
Share This Article