Australia na Saudi Arabia watuma maombi kuandaa Kombe la Dunia 2034

Dismas Otuke
1 Min Read

Australia na Saudi Arabia wametuma maombi ya kutaka kuandaa fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2034.

Hata hivyo, shirikisho la soka barani Asia limetangaza kuwa linaunga mkono ombi la Saudi Arabia kuandaa fainali za Kombe la Dunia mwaka 2034.

Shirikisho la kandanda ulimwenguni, FIFA limetangaza kuwa fainali za mwaka 2030 zitaandaliwa kwa pamoja na mataifa 6 yaliyo katika mabara matatu tofuati.

Mataifa 6 yatakayoandaa fainali za Kombe la Dunia mwaka 2030 yanafuzu moja kwa moja kama wenyeji kushiriki kipute hicho.

Argentina, Uruguay na Paraguay wataandaa mechi tatu za ufunguzi kila taifa likiandaa mchuano mmoja kama sherehe ya kuadhimisha miaka 100, tangu kuanzishwa kwa kipute cha Kombe la Dunia mwaka 1930 nchini uruguay, huku mechi nyingine 101 zikigawanywa katika mataifa ya Uhispania, Morocco na Ureno.

Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2026, zitakazoshirikisha mataifa 48 kwa mara ya kwanza zitaandaliwa kwa pamoja na mataifa ya Marekani, Canada na Mexico.

Share This Article