Aston Villa yamnasa Pau Torres kwa pauni milioni 31 nukta 5

Dismas Otuke
1 Min Read

Klabu ya Aston Villa imetangaza kumsajili beki wa kati wa Uhispania Pau Torres kutoka Villarreal kwa ada ya pauni milioni 31 nukta 5.

Torres,aliye na umri wa miaka 26, aliichezea klabu ya Villareal chini ya kocha Unai Emery kati yam waka 2020 na 2023 na alipiga jumla ya mechi 173 akifunga mabao 12 na pia ameichezeaUhispania mara 23.

Torres alivalia sare ya Uhispania kwa mara ya kwanza mwaka 2019 na alicheza fainali za kombe la euro mwaka 2020 na kombe la duni mwaka 2022.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *