Rais William Ruto amemteua aliyekuwa mbunge wa Starehe Margaret Wanjiru katika wadhfa wa mwenyekiti wa tume ya ustawishaji wa mto Nairobi.
Aliyekuwa waziri msaidizi Millicent Omanga pia ameteuliwa kuwa mwanachama wa tume hiyo.
Ruto amefanya uteuzi huo kupitia kwa gazeti rasmi la serikali la Oktoba 25.
Askofu Wanjiru ameteuliwa kutwaa nafasi hiyo baada ya kumtimua Pamela Olet.
Upande wake Omanga anachukua nafasi ya aliyekuwa Gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu ambaye uteuzi wake ulipingwa mahakamani.