Vijana wa Mikel Arteta walipokea kichapo cha goli moja bila jawabu walicholimbikizwa na miamba wa soka nchini Italia, Inter Milan.
Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Arsenal kupoteza mechi ya kuwania komb la Ulaya, UEFA msimu huu.
Mkwaju waliozawadiwa Inter Milan yamkini kwa njia tatanishi kipindi cha kwanza cha mchezo ulikuwa tosha kuwazamisha Arsenal wakati wa mechi iliyosakatwa katika uwanja wa San Siro jana Jumatano.
Mkwaju huo ulipeanwa kabla ya mapumziko baada ya mchezaji Mikel Merino kuunawa mpira katika eneo la hatari.
Katika mechi zingine zilizosaktwa hiyo jana, wenyeji Red Star Belgrade walinyewa mvua ya magoli 2-5 na Barcelona huku Atlético Madrid ikifunga dakika za lala salama na kuizamisha wenyeji PSG kwa magoli 1-2.