Fainali ya Kombe la Dunia makala ya mwaka 2026 baina ya Uhispania na Argentina katika uwanja wa Metlife mjini New York, itashuhudia aidha Uhispania, wakitwaa Kombe hilo kwa mara ya pili au Argentina watawazwe mabingwa kwa mara ya nne.
Uhispania wamerejea kucheza fainali ya pili tangu waibuke mabingwa mwaka 2010 walipoishinda Uholanzi bao moja kwa bila.
Aidha,Uhispania wamefungwa bao moja pekee katika mechi saba walizopiga.
Upande wao Argentina wanacheza fainali ya saba leo wakitawazwa mabingwa mara tatu;mwaka 1978,1986 na 2022, na kumaliza nafasi ya pili mara tatu mwaka 1930,1990 na 2014.
Argentina ndiyo timu iliyofunga mabao mengi zaidi katika fainali za mwaka huu yakiwa 19, katika mechi saba walizocheza.
Fainali ya Jumapili usiku itakuwa vita kati ya timu yenye ufungaji bora dhidi ya timu yenye safu bora ya ulinzi mashindanoni.
Lionel Messi anategemewa kuongoza mashambulizi ya Argentina wakati Uhispania, wakitegemea huduma za kiungo Rodri kumiliki mpira katika kiungo cha kati .
Argentina itakuwa timu ya tatu kuhifadhi kombe la Dunia baada ya Italia walioshinda mwaka 1934 na 1938 na Brazil walioshinda kombe hilo mwaka 1958 na 1962.
Uhispania inalenga kuwa timu ya nne kushikilia Kombe la Euro na Kombe a Dunia kwa pamoja baada ya West Germany (1972, 1974), Ufaransa (1998, 2000) na pia Uhispania walishinda Kombe la Euro mwaka 2008, kabla ya kushinda Kombe la Dunia mwaka 2010.