Annie Macaulay, aliyekuwa mke wa mwanamuziki wa Nigeria 2Baba Idibia, anaripotiwa kuondoka kutoka kwenye kituo cha kurekebisha tabia ambapo amekuwa akipokea huduma.
Kulingana na watu wake wa karibu ambao hawakutaka kutajwa, kuondoka kwa Annie kutoka kituo hicho hakumaanishi kwamba ametelekeza maisha yake.
Mwigizaji huyo wa filamu za Nollywood alikuwa anatizamiwa kukaa kwa muda mrefu kwenye kituo hicho na sasa anasemekana kupanga namna ya kurejelea maisha yake.
Macaulay amekuwa akikabiliana na matatizo ya kiakili kutokana na matatizo kwenye ndoa yake hali iliyomsababisha aingilie matumizi mabaya ya pombe na dawa za kulevya.
Kabla ya kupelekwa kwenye kituo hicho, 2Baba alikuwa ametangaza kupitia Instagram kwamba wametengana na walikuwa katika harakati za kuhalalisha talaka yao.
Wengi wa wafuasi wake mitandaoni walidhania kwamba akaunti yake ilikuwa imedukuliwa na mtu ambaye aliandika maneno hayo, lakini alichapisha video baadaye akikiri kwamba yalikuwa maneno yake na akaunyi yake haikuwa imedukuliwa na yeyote.
Siku chache baada ya hapo mwanamuziki huyo aliripotiwa kumchumbia Natasha Osawaru.
Inasubiriwa kuona iwapo mama huyo wa watoto wawili atarejelea uhusika wake katika kipindi cha Young, Famous and Africancha Netflix.