Annie Macaulay arejea kwenye mitandao ya kijamii

Amerejea kwenye Instagram ambapo ana wafuasi wapatao milioni 7.9 na kufuta picha zote katika kile kinachoonekana kuwa mwanzo mpya maishani mwake.

Marion Bosire
1 Min Read

Mwigizaji wa filamu za Nigeria Nollywood Annie Macaulay amerejea kwenye mitandao ya kijamii, siku chache baada ya ripoti kuibuka kwamba alikuwa ameondoka kwenye kituo cha kurekebisha tabia.

Annie ambaye ametengana hivi maajuzi na mume wake mwanamuziki 2Baba Idibia hajaonekana kwenye mitandao ya kijamii kwa muda hasa baada ya 2Baba kutangaza utengano wao Januari 26, 2025.

Hatua hiyo ilimwathiri vibaya mama huyo wa watoto wawili ambaye pia anaripotiwa kutatizwa na matumizi ya mihadarati ndiposa akapelekwa kwenye kituo cha kurekebisha tabia.

Sasa amerejea kwenye Instagram ambapo ana wafuasi wapatao milioni 7.9 na kufuta picha zote katika kile kinachoonekana kuwa mwanzo mpya maishani mwake.

Macaulay hata hivyo amebakisha video na baadhi yazo zinamwangazia 2Baba na hajaondoa jina Idibia kutoka kwa jina lake kwenye akaunti hiyo.

2Baba kwa upande mwingine amekuwa akionekana na mpenzi wake mpya Natasha Osawaru, ambaye ni mbunge katika bunge la jimbo la Edo huku akiripotiwa kumchumbia hata kabla ya talaka yake na Annie kukamilika.

Website |  + posts
Share This Article