Amani ya kikanda ni muhimu kwa maendeleo ya taifa hili, asema Mudavadi

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri mwenye mamlaka makuu Musalia Mudavadi.

Kenya  itaendelea kutekeleza ajenda yake ya maendeleo kuhusu amani na usalama, amesema Waziri mwenye Mamlaka Makuu Musalia Mudavadi.

Mudavadi alidokeza kuwa hali ilivyo mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC na Sudan, inahitaji juhudi za pamoja kurejesha hali ya utulivu katika maeneo hayo.

“Kwa sasa nchini DRC, ubaguzi wa kikabila unafanya hali kuwa mbaya zaidi. Raia wa nchi za kigeni wanajipata katika hali tata, na kuhujumu juhudi za kurejesha utulivu,” alisema Mudavadi.

Kulingana na Mudavadi, vita vya muda mrefu nchini DRC na Sudan, vinaendelea kusababisha vifo vya mamilioni ya watu na kuwaacha wengi bila makazi, wanaoathirika zaidi wakiwa watoto, wanawake na wanaoishi na ulemavu.

Waziri huyo wa Mambo ya Nje, alisema mazungumzo ni bora zaidi kuliko makabiliano katika kutafuta amani kwenye nchi zinazokumbwa na mizozo.

Kenya tayari imetoa tahadhari kwa raia wa Kenya wanaoishi DRC, wakitakiwa kuwa makini zaidi kuhusiana na hali ilivyo nchini humo.

Wizara ya Mambo ya Nje imesema itawahamisha raia wa Kenya walio katika nchi zinazokumbwa na mizozo, iwapo hali itabidi kufanya hivyo.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *