Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu Paul Kihara afariki

Kifo cha Kihara kimetangazwa na Jaji Mkuu Martha Koome,  aliyemsifu kwa mchango wake wa kupigiwa mfano katika mfumo wa haki nchini Kenya.

Tom Mathinji
1 Min Read
Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu Paul Kihara, ameaga dunia.

Aliyekuwa Mwansheria Mkuu Paul Kihara, ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 72.

Kifo cha Kihara kimetangazwa na Jaji Mkuu Martha Koome,  aliyemsifu kwa mchango wake wa kupigiwa mfano katika mfumo wa haki nchini Kenya.

“Justice Kihara Kariuki alikuwa mtumishi wa umma aliyejitolea, ambaye mchango wake katika usimamizi wa haki na ukuaji wa taasisi ya kisheria nchini Kenya, utasalia katika historia ya kitaasisi hapa nchini,” alisema Koome.

Kihara aliteuliwa Jaji wa Mahakama Kuu mwaka 2003, kabla ya kupandishwa daraja hadi Mahakama ya Rufaa, ambapo alikuwa Rais wa kwanza wa Mahakama hiyo chini ya katiba ya mwaka  2010.

Alihudumu wadhifa wa Rais wa Mahakama ya Rufaa kuanzia mwaka 2013 hadi mwaka 2018, kipindi ambacho kulingana na Koome, aliimarisha misingi ya kitaasisi ya mahakama hiyo.

Aidha, marehemu Jaji Mstaafu Kihara, alihudumu wadhifa wa Mwanasheria Mkuu nchini Kenya kati ya mwaka 2018 na 2022, akitoa ushauri kwa serikali kuhusu maswala ya kisheria.

Share This Article