Tune ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC), imewakamata muuguzi aliyeajiriwa na serikali ya kaunti Gilbert Suleiman Eskuku, na Mkurugenzi mwenza Abass Abdi Yusuf, katika kampuni moja ya usambazaji bidhaa kwa madai ya ukinzani wa maslahi.
Kulingana na EACC, kampuni hiyo ilipewa zabuni na serikali ya kaunti ya Turkana na kulipwa kitita cha shilingi 2,763,681.
Wawili hao walikamatwa kufuatia kukamilika kwa uchunguzi kuhusu utoaji haramu wa zabuni kwa kampuni hiyo na serikali ya kaunti ya Turkana kati ya mwaka 2017 na 2021.
EACC ilisema kuwa Gilbert Suleiman Eskuku, akihudumu Kama mfanyakazi wa serikali ya kaunti, alitumia kampuni ya Ekwang Suppliers Company Limited, akiwa Mkurugenzi wake pamoja na Abass Abdi Yusuf, kupata zabuni na kupokea malipo kutoka serikali ya kaunti ya Turkana.
Washukiwa hao watafunguliwa mashtaka ya mkimzano wa maslahi, ulanguzi wa pesa na kupata pesa kwa njia ya uhalifu.