Aliyekuwa Afisa Mtendaji wa NHIF, wengine 4 waondolewa doa na mahakama

Martin Mwanje
1 Min Read

Ni afueni kwa Afisa Mtendaji wa zamani wa Hazina ya Kitaifa ya Bima ya Matibabu, NHIF Richard Kerich na washtakiwa wengine wanne. 

Hii ni baada ya watano hao kuondolewa lawama ya kula njama ya kuibia hazina hiyo kitita cha shilingi milioni 116.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo walikuwa ni Ndiba Wairioko, David Kipruto Chingi, Marwa Chacha na Peter Ngunjiri Wambugu.

Katika uamuzi wake, Hakimu Mkuu Mwandamizi Eunice Nyutu alisema upande wa mashtaka ulishindwa kuthibitisha madai dhidi yao katika kesi hiyo ambayo pia ilihusisha kituo cha matibabu cha Meridian.

Walishtakiwa kuhusiana na mpango wa matibabu wa watumishi wa umma pamoja na wanajeshi wenye kima cha shilingi milioni 116.9 uliotolewa kwa kituo cha matibabu cha Meridian.

Wote hao walikanusha madai dhidi yao.

 

 

 

 

 

Share This Article