Katika hatua ya kushangaza, Albania imekuwa nchi ya kwanza ulimwenguni kuteua roboti kuwa waziri.
Roboti hiyo ijulikanayo kama Dieala imeteuliwa kuwa Waziri wa ununuzi wa Umma.
Waziri Mkuu wa Albania Edi Rama alitangaza robi hiyo inayotumia akili mnemba kuwa Waziri, kama njia moja ya kukabiliana na ufisadi.
Albania, ambalo ni taifa dogo lenye idadi ya watu milioni 2.8 pekee, linalenga kukabiliana na ufisadi kabla ya kujiunga na muungano wa Ulaya mwaka 2030.