Andrew Kiptoo Alamisi ameishindia Kenya dhahabu ya kwanza katika siku ya kwanza ya mashindano ya Riadha Duniani, kwa chipukizi walio chini ya umri wa miaka 20 mjini Lima Peru mapema Jumatano.
Kiptoo ambaye ni mshindi mara mbili wa nishani ya fedha katika michezo ya Jumuiya ya madola kwa chipukizi, ameshinda dhahabu katika fainali ya mita 5,000 akisajili muda wa dakika 13 sekunde 41.14 .
Mkenya huyo aliwapiku Abdisa Fayisa wa Ethiopia na Mganda Keneth Kiprop walioshinda fedha na shaba mtawalia.
Mwakilishi mwingine wa Kenya Ishmael Rokitto Kipkurui alimaliza wa nne.
“Nilipoona tumekosa medali katika mbio za wanawake nilisema lazima nitetee nchi.Kwa sasa nuna mwaka mmoja katika mbio za chipukizi, kabla ya kuhamia mbio za watu wazima ambapo napanga kushiriki mita 10,000.”akasema Alamisi
Wakenya Mercy Chepkemoi na Sheila Jebet walimaliza nafasi za 4 na 5 mtawlaia kwenye fainali ya wanawake.
Eisa Medina aliongoza Ethiopia kutwaa nishani za dhahabu na fedha akizikamilisha kwa dakika 14 sekunde 39.79.
Awali jana Sharon Chepkemoi na Diana Chepkemoi walifuzu kwa fainali ya mita 3,000 kuruka viunzi na maji .
Diana Chepkemoi alimaliza wa pili katika mchujo wa pili kwa muda wa dakika 9 sekunde 47.26, huku Sharon Chepkemoi akimaliza wa tatu katika mchujo wa tatu kwa dakika 9 sekunde 7.59.
Bingwa wa Afrika katika mita 800 Sarah Moraa alishinda mchujo wa nne kwa dakika 2 sekunde 51.11 na kufuzu kwa nusu fainali ya kesho.
Hata hivyo Janet Chepkemoi alikosa kufuu kwa nusu fainali, baada ya kuambilia wa mwisho katika mchujo wa kwanza.
Kelvin Kimutai Koech na Phanuel Kosgei pia walifuzu kwa nusu fainali ya mita 800 itakayoandaliwa kesho.
Kimutai alimaliza pili katika mchujo wa 4 huku Kosgei pia akifuzu kwa kuwa na muda bora.
Josphat Kipkirui, Koech Kibiwott, Miriam Chemutai Kibet, and Mary Nyaboke will also compete in the 1500m heats tonight.