Aladwa aondolewa mashtaka ya maandamano

Dismas Otuke
0 Min Read

Mbunge wa Makadara George Aladwa, ameondolewa mashtaka ya kuchochea maandamano yaliyokuwa yamewasilishwa dhidi yake, kufuatia maandamano makubwa ya upinzani yaliyoandaliwa kaunti ya Nairobi Julai mwaka huu.

Jaji Diana Kavedza, alimwondolea mashtaka mbunge huyo pamoja na waakilishi wodi Peter Imwatok wa Makongeni na Moses Ogeto wa Kilimani, na kuagiza warejeshewe dhamana ya shilingi laki moja ambayo kila mmoja alitozwa.

Mahakama pia iliwaomba polisi kutomsumbua mbunge huyo.

Share This Article