Rais wa chama cha Riadha Kenya Jenerali mstaafu Jackosn Tuwei ana imani kuwa mashindani ya kitaifa ya riadha yatarejeshwa katika uwanja wa taifa wa Nyayo, ilivyoratibiwa awali,ili wanariadha wengi wapate fursa ya kufuzu kwa michezo ya Olimpiki.
Kwenye mahojiano ya kipee kupitia KBC ,Tuwei alifichua kuwa wangalia wanajadiliana na usimamizi wa viwanja humu nchini ili mashindano hayo yarejeshwe ugani Nyayo.
“Tungependa kuwa na idadi kubwa ya wanariadha wengi watakaofuzu kwa michezo ya Olimpiki na tungependa kuandaa mashindano ya kitaifa katika uwanja unaotambulika na shirikisho la riadha ulimwenguni,tungali tunazungumza na serikali na tunatumai tutaanda mashindano haya katika uwanja Nyayo jinsi tulivyopanga.”akasema Tuwei
AK imeratibu kuandaa mashindano hayo katika uwanja wa kijeshi wa Ulinzi Sports Complex,ambao hautambuliwi na Shirikisho la riadha ulimwenguni kumaanisha kuwa muda utaosajiliwa hautatumika kufuzu kwa michezo ya Olimpiki.