Afrika kwa Urusi, Urusi kwa Afrika

Martin Mwanje
15 Min Read

Tarehe 29 mwezi Julai, 2023 katika mji wa Saint-Petersburg kulikuwa mkutano kwa kiwango cha juu baina ya Yuri Korobov, Rais wa Jumuiya ya Urusi ya Urafiki na Tanzania, Balozi wa Kibiashara wa “Urusi ya Kibiashara” na Kassim Madjaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Kwa upande wa Tanzania pia kulikuwa Fredrick Ibrahim Kibuta, Balozi wa Tanzania katika Urusi na Balozi na Mbaruk Nassor Mbaruk, Naibu wa Waziri wa Mambo ya Nje. Mwandishi wa habari wa “Toleo Letu” alimwuliza Yuri Korobov kufafanua umuhimu na matokeo ya mkutano wa kilele uliopita siku hizi.

 

Mwandishi wa habari wa “Toleo Letu” (TL): Yuri Anatolyevich, kwanza utoe maneno machache juu ya mkutano wa kilele uliopita…

 

Nia ya urafiki na ushirikiano

 

Yuri Korobov (YK): mkutano wa kilele wa Urusi na Afrika ni mazungumzo ya kiwango cha juu pamoja na wawakilishi wa takriban ujumbe wa nchi za Afrika hamsini. Mkutano huu kulikuwa katika Saint Petersburg tarehe Julai 27-28. Nchi 18 ziliwakilishwa na marais wao, nchi 6 nyingine ziliwakilishwa na mawaziri wakuu na nchi 23 zilishiriki katika mkutano kwa kiwango cha manaibu rais wa nchi au mawaziri. Kwa upande wa Urusi Rais Vladimir Putin alikuwa mwakilishi mkuu. Siku hizi mbili zilikuwa zimejazwa na mazungumzo na mikutano mingi. Mimi kwa naiba ya mwakilishi wa mkutano huu ninaweza kusisitiza kwamba mkutano wa kilele huu uliweka msingi wa mipango mingi ya kimkakati itakayotekelezwa katika miaka ijayo.

 

TL: Unafikiriaje juu ya matazamio ya ushirikiano wa Afrika na Urusi?

 

YK: Nina uhakika kwamba ushirikiano wa Urusi na nchi za Afrika upanue siku za usoni. Tulichonacho sasa? Viungo vya kibiashara wa Urusi na Afrika vinaanza kuibuka: bidhaa za bara la Afrika zinachangia asilimia 3 tu ya mauzo ya nje ya Urusi na asilimia 1 ya bidhaa zinazoagizwa kutoka nje, lakini Afrika inachukua asilimia 20 za ardhi kwenye sayari, inaunda zaidi ya makabila 3000, lugha zaidi ya 2000.

 

TL: Ni ndiyo habari ya kuvutia.

 

YK: Kwa kutumia maneno mawili tu kwa kuelezea michakato inayoendelea, basi labda ningechagua maneno kama “kipekee” na “harambee”. Mila na desturi za nchi zetu ni za kipekee, utamaduni ya nchi zetu ziko kwenye mabara tofauti ni za kipekee, teknolojia zilizoundwa katika hali fulani za hali ya hewa ni za kipekee. Kwa kuunganisha nguvu na kufichua siri ya kuwa “kipekee” kwa kila mmoja tulipata matokeo yanayozidi matazamio ya hesabu yo yote. Mazoea ya kitamaduni, yameng’aa kwa sura mpya na yalisababisha athari ya harambee, ambayo wakazi wa Urusi na nchi za bara la Afrika watapata siku za usoni.

 

TL: Maendeleo ya ushirikiano ni kwa faida ya nani?

 

YK: Jibu kwa swali hili ni dhariri – yananufaisha pande zote! Masoko mapya ya mauzo, teknolojia, mikakati ya muda mrefu ya ushirikiano katika nyanja mbalimbali …Urusi ina ofa nyingi kwa wapatna wa Afrika na Afrika ni ya kuvutia sana kwa Urusi. Tunazungumza sasa kuhusu ushirikiano wa haki unaonufaika Urusi na nchi za Afrika.

 

TL:. Niambie zaidi kidogo, tafadhali.

 

Teknolojia zilizosubiriwa kwa muda mrefu

 

YK: Sasa nitatoa mifano. Tangu kuundwa kwa Jumuiya ya Urafiki ya Urusi na Tanzania mwaka 2021, tuliwahi kubuni na kuanza utekelezaji wa miradi ya pamoja. Baadhi yao ni miradi ya kiuchumi na kitamaduni. Ni muhimu kusisitiza kwamba katika Tanzania tuliungwa mkono katika ngazi ya juu kabisa ya serikali. Miradi yalianza kwa ujenzi wa Nyumba za Urusi katika nchi hii. Wakati wa mkutano wa kilele uliopita siku hizi Rais wetu aliweka kipaumbele umuhimu wa maendeleo ya uhusiano wa kitamaduni kupitia nyumba kama hizi. Kwa upande wa kitamaduni nafiriki mafanikio makubwa ni kuzindua mpango wa kueneza Kiswahili nchini Urusi na Kirusi nchini Tanzania kwa sababu maarifa ya pamoja ya lugha na utamaduni wa nchi-washirika ni ndio msingi wa utekelezaji wa mipango ya kimkakati ya muda mrefu yenye manufaa kwa pande zote katika nyanja mbalimbali, kama jiwe la msingi wa urafiki na upatna wetu.

 

Ushirikiano kama huu uko baina ya nchi zetu na sasa unapanua. Katika mkutano wa kilele ujumbe wa Tanzania ulijumuisha kundi kubwa la wafanyabiashara, na maslahi yao yalihusika ujenzi wa pamoja na usindikaji wa madini ya thamani: maendeleo ya tasnia ya chakula na uzalishi wa chakula kama matunda, maharagwe ya kakao, kahawa na chai; pamoja na utekelezaji wa miradi ya pamoja katika sekta ya nishati, uyeyushi wa madini, mafuta na uchimbaji wa madini (madini ya metali, ikiwa pamoja ni alumini, uendelezaji wa amana za mafuta, gesi na uranium). Wakati wa Forum kulikuwa zaidi ya meza za duara 50 ambapo wafanyabiashara walikubaliana juu ya ushirikiano maalum.

 

Katika mkutano mmoja wa Forum mbele ya Tomas Molelli, afisa ya ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Urusi, wawakilishi wa Tawi la kikanda la Tver “Biashara Urusi”, “Umoja wa Wakulima na Mashamba Binafsi ya Mkoa wa Tver” walisainisha mkataba kuhusu ushirikiano pamoja na kampuni ya kitanzania ya “SSEBO Enterprises Limited” ambayo shughuli kuu ni kilimo cha zabibu, utengenazaji wa mvinyo, uzaloshaji wa zabibu, tangawazi na parachichi.

 

TL: Yuri Anatolyevish, umeshataja teknolojia, unaweza kutoa mifano yo yote?

 

YK: Shukrani kwa Fredrick Ibrahim Kibuta, Balozi ya Tanzania Katika Urusi, Jumuiya ya Urafiki na Tanzania iliandaa mkutano na wawakilishi wa Wizara ya Nishati ya Tanzania na baadhi ya wajasirimali wa Urusi waliofanya kazi katika nyanja ya nishati mbadala. Ni wazi kwamba ikiwa inahitajika kutumia paneli ya jua mahali po pote wa dunia ni ndipo Afrika. Na sasa katika Tanzania asilimia 92 za mfumo wa nishati unaohusika na utumiaji wa mbao kama kuni. Ilikuwa imejadiliwa pia uundaji wa mitambo ya mtandao ya nishati ya jua pamoja na miradi midogo zaidi, kwa mfano, mfumo wa usambazaji wa maji ya moto kulingana na watozaji wa jua au ukuzaji wa vikusanyiko vya joto ambavyo vinaweza kutumika kukausha matunda.

 

TL: Labda utumiaji wa teknolojia kama kizi unaweza kuwa msukumo kubwa kwa maendeleo ya kiuchumi ya Tanzania. Je, kuna teknolojia kama hizi ambazo mtumiaji wa Kirusi atapata?

 

YK: Bila ya shaka, nilikusudia kufafanua kuhusu teknolojia hizi, Tunazungumzia juuya teknolojia na vifaa vya usablimishaji wa bidhaa. Mfumo kama huu ni ya manufaa makubwa kwa suala la kuhifadhi sifa muhimu (hadi 97%) za matunda na kwa suala la usafirishaji kwa sababu kwa njia hii ya kukausha vyakula uzito hupunguzwa hadi asilimia 93 na maisha yasiyo doa ya bidhaa kama hii ni karibu na ukomo; mchakato wa usablimishaji inachukua matumizi madogo ya rasilmali za nishati kulungana na, kwa mfano, mchakato wa kufungia.

 

Wakati wa mkutano wetu Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania, alibainisha teknolojia hii, akiahidi msaada katika utekelezaji na maendeleo yake nchini mwake. Baada ya yote, kulingana na yeye, kufungia-kukausha kunaweza kutatua tatizo muhimu linalohusishwa na uhifadhi wa muda mrefu wa chakula, ambacho bila usindikaji kinapatikana kwa wingi nchini Tanzania. Teknolojia hii itanufaika watengenezaji wakubwa wa Kitanzania na kampuni za kibinafsi. Tanzania ina uwezo mkubwa wa kuchukua sehemu kuu katika soko kuu la kimataifa.

 

TL: Matazamio ni ya kufurahisha sana. Kwa kadiri ninavyoelewa, tunazungumza juu ya usambazaji wa matunda ya bei ya chini kutoka Afrika yanayopelekwa kwenye soko la Urusi, ambapo kila wakati kuna mahitaji ya vitamini na lishe yenye afya.

 

Vituo vya Biashara vya Kimataifa

 

YK: Kuhusu bei ya chini iliyotajwa – si neno la kweli kabisa. Kilo ya bidhaa za aina hii haitakuwa nafuu. Lakini ni muhimu kuzingatia kwamba bidhaa zitakuwa nyepesi sana na kwa hivyo ya kiasi kikubwa, na itapona karibu asilimia 100 baada ya kuwekwa kwenye maji ya kawaida. Kwa njia hii bei ya chini inawezekana. Kusema kweli, ili kufanya matunda ya kitanzania na bidhaa nyingine zilizozalishwa kwa hali ya hewa ya Kiafrika yapatikane zaidi kwa Urusi, Jumuiya ya Urusi ya Urafiki na Tanzania inapanga kuunda nyumba za kibiashara ya Urusi nchini Tanzania na ya Tanzania nchini Urusi siku za usoni. Ni vituo maalum vya ununuzi ambapo kwa kiwango cha makubaliano ya serikali inatolewa msaada wa kina kwa wauzaji wa nje, masuala ya udhibiti wa forodha, uandalizi wa usafirishaji, uhifadhi wa bidhaa, kivutio cha uwekezaji na usimamizi wa kila mchakato yanasuluhishwa. Hii itakuwa msingi wa uhusiano wenye imara tayari.

 

TL: Umeshatajwa Nyumba ya Kirusi na zitabaki na ujenzi wa vituo vya kibiashara kama hivi au zitabadilishwa kuwa kama hizi ya kibiashara?

 

YK: Lakini ni zana tofauti za kuimarisha urafiki wetu. Vituo vya Kibiashara na Nyumba za Kirusi zitakuwepo kwa sambamba. Pamoja na hii ninaamini kwamba ni muhimu pia kufungua balozi zaidi na ofisi za uwakilishi wa nchi za Afrika katika Urusi, katika miji mikubwa, kwa kusambaza vituo vya ushirikiano wa utamaduni na biashara.

 

TL: Kwa wewe wenyewe, mkutano na Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania, ni tukio muhimu zaodi kuliko kushiriki katika mkutano wa kilile, ndivyo?

 

YK: Kila tukio lina umuhimu wa kipekee kwa mimi. Ni muhimu kutaja kwamba tumeshakutana na Waziri Mkuu wakati wa mkutano wa kilele. Kwa hivyo mkutano wetu baada ya mwisho wa Forum unaweza kuchukuliwa kama mwendelezo wa mazungumzo yaliyopangwa. Mikutano ya uso kwa usi na kiongozi wa nchi, jumuiya ya urafiki ambayo ninaongoza, ni muhimu sana na ya heshima sana kwangu. Mkutano huo ulithibitisha nia ya pande zote ya kujenga zaidi ushirikiano imara katika nyanja mbalimbali. Waziri Mkuu alieleza utayari ya kutekeleza mradi huu nchini Tanzania baada ya ukaguzi wa kina na itakuwa kichocheo cha kuunda nafasi ya kufanya kazi pya, kuboresha ustawi wa watu kutoka maeneo ya kipato kidogo hivi leo. Alisisitiza pia kwamba Urusi na Tanzania pamoja nan chi nyingine nyingi za Afrika zina siku za usoni za kiuchumi za pamoja. Na mkutano wa kilele huu ni nafasi kwa kuhakikisha kwamba mimi na wenzangu tunaelekea njia sahihi. Maana hii ni kwamba sisi pamoja ya nchi yetu ambayo inadhai Afrika kuwa bara lenye uwezo mkubwa wa maendeleo katika sekta mbalimbali za uchumi. Ninafurahi kwamba mikutano kama hiyo imepangwa kufanywa kila baada ya miaka mitatu.

TL: Kwa maoni yako, sera ya kuitenga Urusi, iliyofuatwa na Marekani, na nchi kadhaa za Ulaya na zingine, imeathiri kwa kiasi gani kinachotokea?

 

YK: Nina uhakika kabisa kwamba mkutano wa kilele Urusi-Afrika sio matokeo ya vikwazo vyo vyote na shinikizo kutoka kwa maadui wetu wa nje. Huu ni mchakato wa kawaida kabisa wa kuanzisha na kuendeleza mahusiano, ambayo ina mizizi nyuma katika siku za kuwepo kwa Umoja wa Kisovyeti. Baadhi ya masuala ya ushirikiano wetu, kama vile upatikanaji wa chakula au matumizi ya atomi ya amani, yanaweza kuwa makali zaidi. Masuala katika uwanja wa maendeleo ya elimu, biashara, uimarishaji wa uhusiano wa kitamaduni yanaendelea pamoja na njia ya kimkakati iliyoainishwa hapo awali. Leo, kwa kihistoria, hali imetokea wakati mpito kwa kiwango kipya cha ushirikiano umewezekana. Ninaona hii sio matokeo ya vikwazo au shinikizo, naona hii kama mchakato wa kawaida wa mageuzi ya mahusiano kati ya nchi.

 

TL: Asante sana kwa mazungumzo yenye mazao, Yuri Anatolyevich, Kwa kumalizia, nakuomba ueleze kwa ufupi kea wasomaji wetu ni matarajio gani yanaweza kuwa kutokana na maendeleo ya ushirikiano kati ya Urusi na Afrika.

 

YK: Shauku ya mikutano iliyopita, hali ya kujenga ushirikiano na, muhimu zaidi, hatua madhubuti zilizoainishwa wakati wa mazungumzo zinaonyesha kuwa ushirikiano unaendelea kwa kuzingatia maslahi ya pande zote na mipango ya pamoja. Natambua kuwa wajumbe wa Tanzania walikuwa mmoja wa ujumbe mkubwa zaidi katika mkutano wa kilele uliopita. Hii pia ni ishara tofauti. Kwa mara nyingine tena nitaeleza kuhusu vituo vya biashara vya kimataifa ambavyo tunapanga kuunda siku za usoni. Hizi hazitakuwa tu msingi za msaada kwa wafanyabiashara ambao tayari wamehusika katika miradi mbalimbali (pande zote mbili), lakini pia chachu kwa wale wanaoamua kuwekeza katika mahusiano ya Kirusi na Tanzania.

 

Ninaamini kwamba katika Tanzania kupitia Jumuiya ya Urafiki ninawakilisha wote wa Urusi, na kwa hivyo maneno ya shukrani yaliyotolewa na Waziri Mkuu kwenye mkutano wetu lazima nieleze kwa Warusi wote. Na kwa kumalizia nitaongeza kidogo: upende Tanzania, nchi za Kilimanjaro yenye joto na mbali sana, makazi yake ni zaidi ya milioni 70, ambayo iko tayari kunyoosha mkono wa urafiki kwetu. Matunda ya kigeni kutoka Tanzania yafurahishe hila meza. Na ikiwa utapata nafasi, lazima uwe mgeni huko.

Share This Article