Wadau katika sekta ya lishe bora wahimizwa kukumbatia teknolojia

KBC Digital
1 Min Read
Wataalm wa lishe watoa wito wa kukumbatia teknolojia katika lishe bora.

Kongamano la pili la kila mwaka la Kisayansi la chama cha wanafunzi wataalamu wa lishe bora pamoja na wenzao wa vyakula faafu, lilikamilika wikendi, huku miito ya kuthamini matumizi ya teknolojia ikitolewa.

Kongamano hilo lililoandaliwa katika chuo kikuu cha Egerton lilivutia jumla ya vyuo vikuu 16.

Akizungumza wakati wa kongamano hilo, afisa mkuu mtendaji wa taasisi ya wataalamu wa lishe bora na vyakula faafu Dkt. David Okeyo alitoa changamoto kwa wataalamu katika wigo huo kuthamini matumizi ya teknolojia wakati wa kutoa huduma zao ili kuwafikia watu wengi wanaohitaji huduma za lishe bora.

Dkt. Okeyo alisema wataalamu katika sekta hiyo hawajapiga hatua katika matumizi ya teknolojia ambayo alisema ni chombo muhimu katika ustawi wa sekta hiyo.

Rais wa chama hicho George Omollo alisisitiza matumizi ya teknolojia. Alitoa changamoto kwa taasisi za elimu ya juu kujumwisha ujuzi wa programu za kompyuta, matumizi ya akili mnemba pamoja na elimu ya kimsingi ya kompyuta katika programu za mafunzo kuhusu lishe.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *