Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amepongeza mkataba kati ya Israeli na Hamas wa kusitisha mapigano kwa muda wa siku nne.
Kwenye mkataba huo, mateka 50 wa Israeli, watawachiliwa huru na kundi la Hamas, huku Israeli nayo ikiwachilia huru wapalestina 150 wanaozuiliwa katika gereza za Israeli.
Kwenye taarifa Rais Ramaphosa alisema taifa hilo ni mwanachama wa jamii ya kimataijfa inayodhamini amani, haki na udumishwaji sheria ya kimataifa na kwamba taifa hilo lilmefurahishwa na mkataba huo.
Serikali ya chma cha ANC ya Afrika kusini, imekuwa ikiunga mkono vikali Palestina.
Aidha serikali ya Afrika kusini imekashfu vikali mashambulizi ya Israeli dhidi ya Gaza japo Israeli imekuwa ikisisitiza kwamba hatua yake ni ya kujilinda dhidi ya adui wake.
Israeli ilianzisha mashambulizi makali dhidi ya kundi la Hamas katika eneo la Gaza, kufuatia shambulizi la wanamgambo wa Hamas walioingia Israeli na kuwaua watu wapatao 1,200 na kuwateka Nyara wengine 240, tarehe saba mwezi Oktoba mwaka huu.