Afrika Kusini inashiriki uchaguzi wa kitaifa Jumatano Mei 29 ambayo imetanagzwa kuwa siku ya mapumziko .
Wapiga kura milioni 27.7 wamejiandikisha kwa zoezi hilo la kila baada ya miaka mitano ,wakitarajiwa kuchagua bunge jipya,Rais na wakuu wa mikoa 9.
Nchi iliyo tajiri zaidi Afrika ina idadi ya watu milioni 67, huku zaidi ya asimilia 50 wakiishi kwenye ufukara kupindukia.
Afrika Kusini ina manispaa 257 na jumla ya vituo vya kupigia kura 23,292 vilivyosajiliwa .
Rais anahudumu kwa kipindi cha miaka mitano kwa mihula miwili pekee.
Rais,watawala wa mikoa na Wabunge watachaguliwa katika uchaguzi huo mkuu.