Jumla ya wapiga kura milioni 28 waliojisali wanatarajiwa kupiga kura nchini Afrika Kusini katika uchaguzi mkuu wa Mei 29.
Uchaguzi huo utakuwa wa saba katika enzi ya kidemokrasia huku umaarufu wa chama tawala cha African national Congress -ANC, chini ya uongozi wa Rais Ceril Ramaphosa ukididimia kwa kiwango kikubwa.
Wachanganuzi wa kisiasa wamesema ipo haja ya chama cha ANC kubuni serikali ya muungano kutokana na kufifia kwa umaarufu wake.
ANC inakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa chama kipya cha Democratic Alliance na huenda ANC, ikakosa kufikisha asilimia 50 ya kura invyohitajika ili kuunda serikali.
Licha ya kuwa taifa lenye utajiri mkubwa barani Afrika ,Afrika Kusini ingali na idadi kubwa ya watu fukara na pia kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira.