Mabingwa wa Afrika, Afrika Kusini, watafungua harakati za kuwania Kombe Dunia kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 Jumatatu usiku dhidi ya Ufaransa katika kundi E nchini Chile.
Baadaye waakilishi wengine wa Afrika, Nigeria, watakuwa na miadi dhidi ya Norway kundini F.
Morocco ilikuwa timu ya kwanza ya Afrika kupata ushindi baada ya kuinyuka Uhispania mabao 2-0 kundini C Jumapili usiku.