Maafisa wa Tume ya kukabiliana na Ufisadi hapa nchini EACC, wamemkamata na kumfikisha mahakamani afisa wa polisi, kwa madai ya kupokea rushwa.
Konstebo Purity Njeri Kimani kutoka kituo cha polisi cha Kilimani, anadaiwa kupokea shilingi 10,000 kutoka kwa mlalamishi, ili asimfungulie mashtaka ya kukiuka sheria za Trafiki.
Mshukiwa huyo alifunguliwa mashtaka matatu ya kuitisha hongo ya shilingi 20,000 na kupokea shilingi 10,000 ambazo ni sehemu ya pesa hizo.
Hata hivyo alipofika mbele ya Hakimu wa mahakama ya Milimani ya kukabiliana na ufisadi Celesa Okore, mshukiwa huyo alikanusha mashtaka dhidi yake, na aliachiliwa kwa dhamana ya shilingi 20,000. Kesi hiyo itatajwa Aprili 2,2025.