Adele aonyesha pete ya uchumba kwenye tamasha lake

Marion Bosire
1 Min Read

Mwanamuziki wa Uingereza Adele alionyesha pete yake ya uchumba alipokuwa akiendelea kutumbuiza jukwaani kwenye tamasha lake.

Mwimbaji huyo ambaye pia ni mwandishi wa nyimbo aliingia jukwaani huko Nevada Las Vegas nchini Marekani Ijumaa usiku akiwa na furaha.

Alipokuwa akiimba wimbo wake uitwao ‘I Drink Wine’ Adele aliinua mkono wake juu na kuonyesha pete ishara ya kutaka kutangaza uchumba wake na mpenzi wake Rich paul.

Baada ya kutangaza uchumba wao mwezi Agosti mwaka huu, adele amekuwa akionyesha pete yake kwenye matamasha ishara kwamba anampenda Paul.

Kabla ya kuingia kwenye mahusiano na Paul, Adele alikuwa kwenye ndoa na Simon Konecki kati ya mwaka 2018 na 2021 ila uhusiano wao ulianza mwaka 2011 na wana mtoto wa kiume aliyezaliwa mwala 2012.

Website |  + posts
Share This Article