Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi nchini, EACC ina Afisa Mkuu Mtendaji mpya.
Hii ni baada ya Abdi Mohamud kuapishwa leo Jumatatu asubuhi kuchukua wadhifa huo katika hafla iliyofanyika katika Mahakama ya Juu.
Hafla hiyo iliongozwa na Jaji Mkuu Martha Koome.
Mohamud anajaza pengo lililoachwa wazi na Twalib Mbarak ambaye aliondoka kwenye wadhifa huo baada ya muhula wake wa kuhudumu wa miaka 6 kufikia kikomo.
Mwenyekiti wa EACC David Oginde na Mkurugenzi wa Idara ya Upelelezi wa Jinai, EACC Amin Mohamed ni miongoni mwa waliohudhuria hafla hiyo.
Mohamud anatarajiwa kuwa mstari wa mbele kuimarisha vita dhidi ya zimwi la ufisadi ambalo kufikia sasa limesababisha nchi kupoteza mabilioni ya fedha za maendeleo.