Simba SC kufungua Ligi ya Afrika AFL kuanza Ijumaa Dar

Dismas Otuke
1 Min Read

Makala ya kwanza ya kipute cha kuwania ligi ya Afrika baina ya  vilabu maarufu kama Africa Football League  (AFL), yatang’oa nanga Ijumaa, kwa robo fainali ya kwanza kati ya mabingwa mara 10 wa ligi ya mabingwa Al Ahly kutoka Misri dhidi ya  Simba SC ya Tanzania kuanzia saa kumi na mbili jioni.

Pambano hilo litapigwa katika uchanjaa wa Benjamin Mkapa na kuhudhuriwa na Rais wa Shirikisho la Soka Ulimwenguni, FIFA Giani Infantino na Kinara wa Shirikisho la Soka Afrika,  CAF Dkt. Patrice Motsepe miongoni mwa viongozi wengine wa soka.

Petro Luanda ya Angola itawaalika Mamelodi Sundowns Jumamosi na robo fainali mbili za mwisho zipigwe Jumapili, Esperance Du Tunis ikiwa ziarani Kinshasa dhidi ya TP Mazembe,  huku Enyimba wakimaliza udhia na Wydad Casablanca kutoka Morocco.

Mshindi wa kombe hilo atatuzwa dola milioni 4 za Marekani, nafasi ya pili milioni 2.8 na timu zitakazofuzu kwa nusu fainali zitapokea dola milioni 1.7 kila moja.

 

Website |  + posts
Share This Article