Prisons Kenya watwaa ligi kuu Voliboli baada ya miaka 7

Dismas Otuke
1 Min Read

Prisons Kenya walitawazwa mabingwa wa ligi kuu ya Voliboli kwa wanaume kwa mara ya kwanza baada ya subira ya miaka 7 kufuatia ushindi wa seti 3-2, dhidi ya mabingwa watetezi General Service Unit, Jumatano usiku katika uwanja wa Kasarani .

Prisons walinyakua seti za kwanza mbili
pointi 25-20, 25-21 na kupoteza seti zilizofuatia mbili 22-25, 28-30 na kulazimu mechi kuamuliwa katika seti ya tano na ya mwisho waliyoshinda alama 15-10.

Historia pia iliandikwa upya kwa wanawake ambapo Kenya Commercial Bank waliipakata Kenya Pipeline seti 3-1 na kutawazwa mabingwa kwa mara ya kwanza baada ya subira ya miaka 15.

Share This Article