Zaidi silaha 700 haramu zimetwaliwa katika Kaunti ya Turkana, kufuatia oparesheni kali inayoendelea katika Kaunti hizo mbili.
Oparesheni nyingine katika kaunti ya Pokot Magharibi pia ilifanikisha kutwaliwa kwa silaha nyingine 339.
Akizungumza wakati wa ziara yake katika Kaunti ya Turkana ya kutathmini hali ya usalama Mratibu wa eneo la Bonde la ufa Abdi Ali Hassan alisema licha ya silaha hizo kurejeshwa, operesheni ya kuwapokonya raia na majangili silaha itaendelea bila mapendeleo katika Kaunti zote mbili.
Aidha, amewaonya wale ambao bado wanamiliki silaha hizo haramu kuzirejesha kwa serikali, la sivyo serikali itaendelea kutumia nguvu kuwapokonya.
Haya yanajiri huku Rais William Ruto akitarajiwa kuzuru Kaunti hiyo wiki ijayo kwa ziara ya maendeleo na uzinduzi wa usafirishaji wa mafuta ya Turkana.