Marekani imemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Usalama wa Mtandao Sean Cairncross, kufuatia hitilafu kubwa za mtandao zilizokumba taifa hilo zilizodaiwa zilisababishwa na akili unde(AI).
Kulingana na vyanzo vya habari nchini humo, hatua ya kutimuliwa kwa mkurugenzi huyo pia ziliungwa mkono Rais wa Marekani Donald Trump, akisema Cairncross hakuwa na tajiriba ya kutekeleza majukumu hayo.
Ikulu ya White imesema kuwa majukumu yake sasa yatatekelezwa kwa muda na Kirsten Davies, ambaye ni Afisa Mkuu wa Teknolojia ya Habari katika Wizara ya Ulinzi.
Kusimamishwa kazi kwa Cairncross, kumejiri baada ya taifa hilo kukumbwa na hitilafu za mtandao ambazo ziliathiri safari za ndege, huduma za benki, teknolojia za kampuni kama vile Microsoft na Apple, na mifumo ya Usalama wa Taifa.
Baada ya kuteuliwa kwa Davies kuchukua wadhifa huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio, alimpongeza Davies akisema analenga kufanya kazi pamoja naye ili kuboresha usalama wa mtandao wa Marekani.
Kabla ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Usalama wa Mtandao wa Taifa, Cairncross alihudumu katika nyadhifa mbalimbali ndani ya Ikulu ya White House wakati wa muhula wa kwanza wa utawala wa Trump.