Washikadau katika sekta ya sukari wanatoa wito kwa serikali kuweka udhibiti mkali wa uagizaji sukari, hasa kupitia maeneo ya kuingia nchini ya Malaba na Busia.
Wakiongozwa na Meneja wa shughuli za kampuni ya Mumias Stephen Kihumba, wameelezea wasiwasi wao kuhusiana na ongezeko la sukari inayoagizwa nchini.
Akiwahutubia wanahabari mjini Busia, Kihumba alisema ongezeko la uagizaji bidhaa hiyo katika kaunti za mpakani linadhuru wakulima wa miwa wa maeneo hayo na kutishia ukuaji wa sekta ya sukari nchini.
Amewahimiza wakulima kukumbatia kilimo cha miwa akiongeza kuwa zao hilo lina uwezo wa kuboresha mapato ya familia zao na kufufua sekta ya sukari nchini.
Taarifa ya Sayyid Abdalla