Viongozi zaidi ya 140 kutoka mataifa mbalimbali wako jijini New York, Marekani kuhudhuria kikao cha 78 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA.
Kikao hicho kitaanza kesho Jumanne huku ajenda yake kuu ikiwa ni kujadili vita vya Urusi nchini Ukraine na mabadiliko ya tabia nchi.
Viongozi wa mataifa wanachama wa Umoja wa Mataifa, UN pia wanatarajiwa kuwasilisha maoni na matakwa yao kuhusu mambo ya dharura ambayo wangetaka ushirikiano au usaidizi kutoka kwa UN.
Rais William Ruto wa Kenya ni miongoni mwa viongozi waliopo nchini Marekani kuhudhuria kikao hicho.