Kenya yachaguliwa tena katika Baraza la ITU

Kenya ilikuwa miongoni mwa mataifa 19 ya Afrika, yaliyowania viti 13 vilivyotengewa bara hilo.

Tom Mathinji
1 Min Read
Kenya imechaguliwa tena kwa Baraza la ITU

Kenya imechaguliwa tena kwenye Baraza la Chama cha kimataifa  Mawasiliano ya Simu (ITU) kwa kipindi kipya cha miaka minne, baada ya kupata kura 136 kati ya kura 173 zilizopigwa.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Dijitali William Kabogo, alitangaza hayo baada ya mkutano wa ITU ulioandaliwa Doha, Qatar, ambapo Kenya ilipata nafasi kwenye baraza hilo kwa muhula wa mwaka  2027-2030.

Kenya ilikuwa miongoni mwa mataifa 19 ya Afrika, yaliyowania viti 13 vilivyotengewa bara hilo.

Côte d’Ivoire iliibuka ya pili kwa kura 135, Senegal ilipata 134 huku Tanzania ikirithika na kura 131, kulingana na matokeo rasmi ya uchaguzi huo.

Kulingana na Kabogo, jukumu hilo jipya litatoa fursa kwa Kenya kuendelea kutoa mchango wake kwa uongozi wa chama hicho, ikiwa ni pamoja na utoaji maamuzi kuhusu mpango wa kifedha wa mwaka  2028–2031.

“Katika baraza hilo, Kenya itashinikiza uunganishaji nafuu, ujuzi wa kidijitali, uaminifu kwenye huduma za dijitali na sauti dhabiti ya Afrika kuhusu sera za Kimataifa za ICT,” alisema Kabogo.

Share This Article