Rais wa Gambia Musa Ceesay alipachika bao pekee na la ushindi dhidi ya Mombasa United, kunako kipindi cha kwanza na kuwasaidia AFC Leopards kupanda hadi nafasi ya tatu ligini.
Ceesay alipachika bao hilo katika dakika ya 42 katika uwanja wa Wang’uru na kuwapa ushindi wa tatu ligini msimu huu.
Katika matokeo mengine Police FC wakiwa nyumbani ugan Police Sacco DT walipata ushindi wa 2-1 dhidi ya matarishi Posta Rangers,Kusi Nana Asanta na Erick Zakayo wakipachika magoli ya wenyeji naye Mark Shaban akajibu moja kwa wenyeji.
Murang’a Seal wakiwa nyumbani waliduwazwa baada ya kupigwa 2-1 na Mathare United,Victor Omune akifunga mabao yote naye Michael Owen akafunga la kufutia machozi kwa wenyeji.
Kakamega Homeboyz waliambulia sare tasa dhidi ya viongozi wa ligi hiyo Kenya Commercial Bank.