Bingwa wa dunia katika mbio za mita 3,000 kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 Emmanuel Kiprono, ameteuliwa kuwania tuzo ya mwanariadha chipukizi bora wa mwaka huu.
Kiprono ambaye pia alinyakua nishani ya fedha ya dunia katika mbio za nyika mapema mwaka huu, aliweka muda wa pili wa kasi katika mbio za mita 3,000 mjini Oregon Marekani Agosti,aliposhinda kwa dakika 7 sekunde 27.28.
Kiprono ameteuliwa kuwania tuzo hiyo pamoja na Cooper Lutkenhaus na Tate Taylor wote wa Marekani.
Mshindi wa tuzo hiyo atatangazwa Novemba 29 mjini Monaco,Ufaransa.