Kisiwa cha Cape Verde chaandaa uchaguzi wa Urais

Dismas Otuke
1 Min Read
Kisiwa cha Cape Verde kimeandaa uchaguzi wa Urais siku ya Jumapili huku wapinzani watano wakijitosa ulingoni dhidi ya Rais aliye mamlakani José Maria Neves.
Miongoni mwa wanaowania kiti hicho ni  waziri wa zamani wa haki  Joana Rosa,anayepania kuwa Rais wa kwanza wa kike nchini humo.
Mshindi ni sharti apate zaidi ya asilimia 50 ya kura, la sivyo duru ta pili itaandalwia baada ya majuma mawili.
Neves anawania muhula wa pili  baada ya kuzoa asimilia 52 katika uchaguzi uliopita.
Taifa hilo lililopata uhuru wake mwaka 1975 kutoka kwa Ureno, lina idadi ya watu wapatao nusu milioni.

 

Share This Article