Mlinzi wa timu ya taifa ya Uganda Khalid Aucho amestaafu ramsi kutoka soka ya kimataifa baada ya kuichezea Uganda Cranes kwa kipindi cha miaka 13.
Khaucho alifanyiwa sherehe ya kuamuaga rasmi punde baada ya sare ya bao moja kati ya Cranes na Zebras kutoka Botswana Jumamosi jioni katika uwanja wa Hoima City viungani mwa jiji la Kampala.
Mwanandinga huyo aliye na umri wa miaka 33 ambaye pia amewahizichezea Tusker FC na Gor Mahia za Kenya,alicheza jumla ya mechi 78 akiwa na Cranes kuanzia mwaka 2013 na kufunga mabao mawili.
Hafla ya kumuaga iliandaliwa punde baada ya mechi ya kundi H kufuzu kwa fainali za Kombe la mataifa ya Afrika mwaka ujao dhidi ya Botswana Jumamosi jioni.