Watatu wafariki,11 wajeruhiwa kufuatia kuporomoka kwa ukuta Nairobi

Dismas Otuke
1 Min Read

Watu watatu wameripotiwa kuaga dunia na wengine 11 kujeruhiwa kufuatia kuporomoka kwa ukuta katika eneo la Riverside kaunti ya Nairobi mapema Jumamosi.

Ukuta huo uliokuwa ukijengwa uliporomoka Jumamosi asubuhi na kuwaangukia watu  waliokuwa wakiujenga.

Kulingana na taarifa kutoka kaunti ya Nairobi watu wengine wanane bado hawajulikani waliko kufuatia mkasa huo uliotokea mida ya saa tano unusu asubuhi.

Jumla ya wajenzi 39 walikuwa wakijenga ukuta huo huku 22 wakiwa wamebainishwa  waliko wakiwemo majeruhi 11 na watatu waliofariki huku  wengine bado hawajulikana waliko.

 

 

Share This Article