Akanor atawazwa kocha bora Oktoba

Dismas Otuke
1 Min Read

Kocha wa mabingwa watetezi wa ligi kuu Kenya, Gor Mahia, Charles Akanor ametawazwa mkufunzi bora wa mwezi Oktoba.

Akanor, ambaye ni raia wa Ghana, alimeshinda tuzo hiyo baada ya kuwaongoza K’ogalo kushinda mechi nne za ligi kuu mwezi jana.

Gor walifungua ligi kwa ushindi wa 4-2 dhidi ya Murang’a Seal, kabla ya kuwalemea APS Bomet, Bandari na Kakamega Homeboyz bao  1-0 kila moja.

Kando na kutoshindwa mwezi jana, Gor waliongoza jedwali la ligi kwa kudumisha asilimia 100.

Share This Article