Jumla ya mataifa 39 yatakayoshiriki fainali za 23 za Kombe la Dunia mwaka huu yatakita kambi ya mazoezi nchini Marekani.
Timu zingine saba zitakita kambi yao ya mazoezi nchini Mexico, huku zingine mbili zikiwa nchini Canada.
Kipute cha Kombe la Dunia kitaandaliwa kati ya Juni 11 na Julai 19, huku jumla ya mechi 104 zikichezwa katika miji 16 tofauti.
Marekani itaandaa mechi 78 huku Canada na Mexico zikigawana mechi 13 kila moja.
Fainali itachezwa Julai 19 katika uwanja wa Metlife katika jimbo la New York.