Serikali imetangaza kumtuza kila mchezaji wa timu ya taifa ya raga ya Kenya ya chipukizi saba upande iliyoshinda dhahabu ya Olimpiki shilingi robo milioni kwa ufanisi wake.
Katibu katika wizara ya Michezo Elijah Mwangi, alitangaza haya alipoandaa dhifa ya chakula cha jioni Jumamosi usiku kusherehekea ushindi huo.
Kenya almaarufu Lionesses ilishinda dhahabu ya raga kwa wachezaji saba upande katika makala ya nne ya michezo ya Olimpiki kwa chipukizi yanayoendelea nchini Senegal.
Lionesses iliwahsinda Australia alama 17-12, kupitia muda wa ziada na kutawazwa mabingwa ,ikiwa historia kuwa timu ya kwanza kutoka Kenya kushinda dhahabu ya timu katika Olimpiki.