The Flamingoes ya Nigeria watashuka katika uwanja wa Mohammed VI nchini Morocco, dhidi ya Japan,katika fainali ya Kombe la Dunia kwa wasichana chini ya umri wa miaka 17.
Fainali hiyo itatanguliwa na mechi ya kuwania nishani ya shaba baina ya Brazil na mabingwa watetezi Korea Kaskazini.
Nigeria watamenyana na Japan kuanzia saa tatu unusu,waakilishi wa Afrika wakiwinda taji ya kwanza nao Japan wakiwania kombe la pili.
Nigeria walifuzu kwa fainali baada ya kuwadhalilisha Brazil mabao 4-1 nao Japan wakawabwaga Korea Kaskazini mgoli 4-1 kufuatia sare ya 1-1.