Prof. Phoebe Okowa achaguliwa katika Mahakama ya ICJ

Okowa alichaguliwa kwenye mahakama hiyo pamoja na Dapo Akande wa Uingereza, François Alabrune wa Ufaransa, Mahmoud Daifallah Hmoud kutoka Jordan na Rena Lee wa Singapore.

Tom Mathinji
1 Min Read
Prof. Phoebe Okowa.

Profesa Phoebe Okowa amechaguliwa kuwa Jaji kwenye Mahakama ya Kimataifa kuhusu Haki (ICJ), wadhifa atakaohudumu kwa kipindi cha miaka tisa ijayo.

Prof. Okowa aliibuka mshindi baada ya kupata kura 183 kutoka kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kura 13 kutoka kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na kuwapiku washindani wake kutoka mataifa mengine, akiwemo mwaniaji kutoka Sierra Leone, Charles Chernor Jalloh.

Okowa alichaguliwa kwenye mahakama hiyo pamoja na Dapo Akande wa Uingereza, François Alabrune wa Ufaransa, Mahmoud Daifallah Hmoud kutoka Jordan, na Rena Lee wa Singapore.

Profesa huyo atakuwa miongoni mwa Majaji 15 ambao wamejukumiwa kusuluhisha mizozo baina ya nchi na kutoa ushauri kuhusu masuala ya sheria ya kimataifa.

Kuchaguliwa kwa Prof. Okowa katika mahakama hiyo ni hatua kubwa kwa uwakilishi wa Kenya katika uongozi wa mahakama kwenye ngazi ya kimataifa.

Okowa ni wakili na Profesa wa sheria ya kimataifa.

Share This Article